ProZ.com translation contests »
32nd Translation Contest: "Movie night" » English to Swahili » Entry by Geofry Irungu


Source text in English

Translation by Geofry Irungu (#37084)

To say that I was compelled by Parasite from start to finish is an understatement; its filming style with tracking shots are enthralling. Having watched several Korean films during the London Korean Film Festival, I was familiar with the usual genres employed in such films but Parasite seemed to defy them all! Parasite is comedic, in a quirky way, it is also a thriller, straddles class divisions and also depicts a family tale amongst other genres and is therefore likely to appeal to all ages.

Parasite truly deserves to be watched in a cinema to appreciate its nuances and the stylish cinematography. As a summary, to avoid spoilers, Parasite tells the tale of the interaction between the Park family and the Kim’s, an unemployed family, whose contrasting worlds collide with long lasting consequences.

[...]Bong Joon-Ho manages to pique the audience’s interest with brightly lit shots coupled with the effective use of indoor space, and it is surprising to realise, after the film’s 2 hour 12 minute length, that most of the scenes occur within the Park family’s home. The mundane elements of domesticity are displayed with an intriguing perspective showcasing Bong Joon-Ho’s flair. It is a slow burner but you will revel in its beauty and ingenuity as Parasite convinces that it operates solely on one level but it is in fact multi-layered and depicts social realism with empathy and pathos.

The cast are beguiling to watch, every facial movement and action is accentuated, even the mere act of walking up or down stairs can convey hidden meaning, which the camera fragments. Levels of unease are also created by virtue of that effective use of space with unusual camera angles and dramatic weather conditions ratcheting up that sensation. There is a surreal nature to Parasite, which its score emphasises, and furthermore the film adopts elements of the absurd devised in such an ingenious way which is truly cinematic magic. Parasite’s apparent eeriness will certainly keep you riveted and would not feel alien to the Twilight Zone school of filmmaking.

The actors are very impressive and add breadth to their roles creating relatability whilst seeming effortlessly cool. When Ki-Woo and Ki-Jeong Kim were working within the Park family home as private tutors they certainly epitomised this level of nonchalant, understated authority creating an aura of mysticism with the unspoken, almost mythical, tutoring techniques employed. Quite simply, the actors Park So-Dam and Choi Woo-Sik, as Ki-Woo and Ki-Jeong, are compelling to watch in the different directions that Parasite follows and they carry these performances seamlessly thereby inviting the audience to be on their side.

[...]Parasite is a remarkable piece of extremely skilful filmmaking, it is simply a must see film, and so I am looking forward to re-watching the film on its UK general release date.
Kusema kwamba nilivutiwa na Parasite kutoka mwanzo hadi mwisho ni kusema kidogo; mtindo wake wa uchukuzi na kurekodi ni wa kuvutia. Baada ya kutazama filamu kadhaa za Kikorea wakati wa Tamasha la Filamu la Kikorea la London, nilikuwa na ufahamu wa aina za kawaida zinazotumika katika filamu hizo, lakini Parasite ilionekana kuzipuuza zote! Parasite ni ya kuchekesha, kwa njia ya kipekee, pia ni ya kutisha, inavuka mipaka ya tabaka na pia inaonyesha hadithi ya familia miongoni mwa aina nyinginezo, na kwa hiyo inaweza kukubalika na watu wa umri wote.

Parasite inastahili kabisa kutazamwa sinemani ili kuthamini undani wake na uandaji sinema wa kuvutia. Kwa mukhtasari, ili kuepuka kuharibu uhondo, Parasite inasimulia hadithi ya mwingiliano kati ya familia ya Park na Kim, familia isiyokuwa na ajira, ambazo ulimwengu wao tofauti unagongana na matokeo makubwa ya kudumu.

Bong Joon-Ho anafanikiwa kuchochea hamu ya hadhira kwa picha zenye mwangaza mzuri zinazounganishwa na matumizi yenye ufanisi wa nafasi za ndani, na ni kushangaza kugundua, baada ya muda wa filamu wa saa 2 na dakika 12, kwamba sehemu kubwa ya matukio yanatokea ndani ya nyumba ya familia ya Park. Mfumo wa kawaida wa maisha ya ndani unaonyeshwa kwa mtazamo wa kuvutia ukionesha ustadi wa Bong Joon-Ho. Ni filamu yenye mwendo wa pole, lakini utafurahia uzuri wake na ubunifu huku Parasite ikionyesha kwamba inafanya kazi kwa kiwango kimoja tu, lakini ukweli ni kwamba ina tabaka nyingi na inaonyesha ukweli wa kijamii kwa hisia na huruma.

Wasanii wanavutia kutazama, kila mwendo wa uso na hatua unasisitizwa, hata tendo la kawaida la kupanda au kushuka ngazi linaweza kueleza maana iliyofichika, ambayo kamera inagawa. Viwango vya wasiwasi pia vinajengwa kwa kutumia nafasi hiyo kwa kutumia pembe za kamera zisizo za kawaida na hali ya hewa ya kuvutia ikiongeza hisia hizo. Kuna asili ya kipekee katika Parasite, ambayo ala yake inasisitiza, na zaidi ya hayo, filamu inachukua vipengele vya upuuzi vilivyoundwa kwa njia ya akili ambayo ni uchawi wa kweli wa sinema. Kutisha kwa wazi kwa Parasite bila shaka itakufanya uwe makini na hautahisi kama kitu cha ajabu katika shule ya kutengeneza filamu ya Twilight Zone.

Wasanii wanavutia sana na wanaweka upana katika majukumu yao, wakiongeza uhusiano wa kuvutia huku wakionekana kuwa wa kuvutia bila jitihada. Wakati Ki-Woo na Ki-Jeong Kim walipokuwa wakifanya kazi ndani ya nyumba ya familia ya Park kama walimu binafsi, kwa hakika walitafsiri kiwango hiki cha mamlaka kwa kutojali, wakiunda anga ya siri na njia za kufundishia zisemwazo, zenye hadithi karibu na mithili ya uwazi. Kwa ufupi, wasanii Park So-Dam na Choi Woo-Sik, kama Ki-Woo na Ki-Jeong, wanavutia kuangaliwa katika mwelekeo tofauti ambao Parasite inafuata, na wanachukua hizi michezo kwa urahisi, hivyo kuwaalika wasikilizaji kuwa upande wao.

Parasite ni kipande cha filamu kinachovutia sana kilichotengenezwa kwa ustadi wa hali ya juu, ni filamu ambayo lazima uione, na kwa hiyo ninatarajia kutazama tena filamu hiyo siku ya kutolewa rasmi nchini Uingereza.


Discuss this entry