Kutoka ''Kwani mashine ya mawazo imeharibika? kutoka kwa Mwanauchumi
Nyakati za Maongozeko zimerudi katika bonde la Silikoni. Maegezo ya ofisi kando na barabara kuu ya 101 yamepabwa tena na insiginia ya biashara mpya zenye matumaini. Kodi zinapanda, kama ilivyo mahitaji ya nyumba za likizo katika miji ya mapumziko kama vile Ziwa la Tahoe, ishara ya utajiri unaojiri. Sehemu ya Kidaka ilikuwa mahali pa kuzaliwa pa kiwanda cha nusukondakta na tarakilishi na viwanda vya mitandao ambavyo vimekua baada ya kuzinduliwa. Wataalamu wake walitoa maajabu mengi yanayofanya dunia kuhisika kama ya siku za usoni, kutoka simu za skrini -za mguso hadi uchunguzi wa papo hapo wa maktaba kuu na nguvu za kuendesha ndege isiyo na mwendeshaji kwa umbali wa maelfu ya maili. Ufufuo katika shughuli zake za biashara unadokeza kuwa kuna maendeleo.
Kwa hivyo inaweza kushangaza kwamba baadhi ya wakazi hufikiria kuwa Bonde la Silikoni limezembea, na kwamba kiwango cha uvumbuzi kimekuwa kikilegezwa kwa miongo sasa. Peter Thei, mwasisi wa paypal, na mwekezaji wa kwanza wa kutoka nje katika Facebook, anasema kuwa uvumbuzi kule Marekani ni, ''huwa kati ya mahali mahututi na kifo''. Wahandisi kutoka nyanja zote wanakubaliana na maoni haya ya kutamausha. Na kikundi kidogo lakini kinachokua cha wanauchumi kinadhani kwamba athari za kiuchumi za uvumbuzi wa leo zitaongezeka zikilinganishwa na zile za zamani.
[...]
Kutoka pande zote, uvumbuzi unaowezeshwa na matumizi ya nguvu rahisi umevuma. Tarakilishi zimeanza kuelewa lugha ya kibinadamu. Watu wanadhibiti michezo ya video kupitia kwa miondoko ya mwili pekee- teknolojia ambayo hivi karibuni inaweza kupata programu-tumizi katika dunia ya biashara. Uchapaji wa pande tatu unaweza kusaga mkusanyiko wa vitu tata ambazo zinazidi kuongezeka, na hivi karibuni utaweza kutumiwa kwa tishu za bianadamu na kwa mabaki ya mimea na wanyama.
Mtu anayepinga uvumbuzi anaweza kuyapuuza haya kama''kesho iliyosongamana''. Lakini wazo kwamba maendeleo yanayoongozwa-na teknolojia lazima yaendelee bila kukoma au yaendeleee kufifia, badala ya kupungua na kutiririka, kinyume na historia. Chad Syverson wa Chuo Kikuu cha Chicago anaelezea kwamba ukuaji wa kiutendaji katika enzi za umeme ulibumbuasa. Ukuaji ulipungua katika kipindi cha uvumbuzi muhimu wa vitu vya umeme mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, halafu ukaongezeka.