"Nina pendekezo." Ilinisogelea kwa karibu kama rafiki angu April afanyavyo pindi anapotaka kuniambia siri, japo kuwa siri zake hazinaga mashiko. Na huwa sio siri hata. _" kama hutomwambia mtu niko hapa, nita kuponya macho yako."
"Toka kwenye huu mji!"
Kikapepesa macho mara kadhaa, "hicho ndio nacho jaribu kufanya."
"Ninacho maanisha ni kwamba huwezi kufanya hivyo."
"Kwanini haiwezekani?"
"Kwanza, hakuna mtu ameweza kuponya macho yangu , pasina miwani."
"Mimi ninauwezo wakipekee, nitakuonyesha kama tu..."
"....Nisipo mwambia mtu yoyote kuhusu wewe."
"Hilo ndilo sharti la muhimu zaidi ,hicho ndo kiini."
"Nitajuaje kama huto nipofua ?" Unaweza kuwa miongoni mwa hao matapeli wanaotoa ahadi za uwongo."
Kiliendelea kusisitiza . "Sito weza kufanya kitu kama hicho kwa kiumbe ambaye hajanidhuru kwa lolote."
"Unamaanisha kama ningekudhuru ungenifanya niwe kipofu?"
"Hilo siwezi kusema kwa sasa"
"Na ukiyaponya macho yangu, na nisipomwambia mtu yoyote kuhusu wewe, utaondoka katika eneo letu."
"Hilo nakuhakikishia."